Faragha ni kulinda kile kinachotufanya kuwa binadamu: tabia zetu za kila siku, utu wetu, hofu zetu, mahusiano yetu, na kuathirika kwetu. Kila mmoja anastahili faragha. Umoja wa mataifa ulipitisha na kratibu faragha kama haki ya kibinadamu katika Azimio la Ulimwengu la Haki za Kibinadamu mwaka 1948. Hatahivyo, serikali, mashirika, na mamlaka nyingine mara nyingi hutuzuia kutimiza haki yetu ya faragha kwa kufanya ufuatiliaji,kuchukua taarifa na kutudhibiti.
Wanaharakati, watetezi wa haki za binadamu,walio wachache na watu wanaopinga kuhusu maendeleo mara nyingi hulenga ufuatiliaji huu, hivyo wana mtazamo wa kipekee juu ya umuhimu wa faragha na kutojulikana mtandaoni.
Katika toleo hili la PrivChat, tunawaweka pampja wataalamu wenye uzoefu katika uharakati au kufanya kazi na makundi ya wanaharakati ambao wataongelea uzoefu waloionao katika kufuatilkiwa na faragha:
JiungeAli Gharavi, Mtaalamu mkuu wa Programme, Swedish International Development Agency; Nadya Tolokonnika, wasanii, wanaharakati, na wanachama waanzilishi wa Pussy Riot; naNicholas Merrill, mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji, chu cha Calyx kujadili uzoefu katika ufuatiliaji na kwa nini kupigania faragha ni jambo muhimu katika kuhakikisha haki za binadamu kwa wote.
Cindy Cohn, Mkurugenzi mtendaji wa EFF, atajiunga nasi kama muwezeshaji na msimamizi.